Ujana Salama
Mradi wa nyongeza ya fedha (cash plus) unaohusu ustawi na mabadiliko salama kwa vijana - Matokeo ya tatihimini ya kati

Publication series:
Innocenti Research Briefs
Download the report
(PDF, 1.05 MB)(PDF, 1.04 MB)
Related Project(s):
Abstract
Mradi huu wa majaribio wa ‘Cash Plus’ unaohusu
Ustawi na Mabadiliko Salama na Yenye Afya kwa Vijana
nchini Tanzania, kwa ufupi “Ujana Salama”, unalenga
kuimarisha maisha ya vijana wa vijijini. Vijana hawa wa
umri wa balehe wanatoka katika kaya maskini na
wanakabiliwa na hatari nyingi za kiafya na kiuchumi.
Mradi huu unatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii Tanzania (Tanzania Social Action Fund (TASAF)) na
kuendeshwa kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
(Productive Social Safety Net (PSSN)). Mpango huo
unawalenga vijana wa umri wa balehe katika kaya
zinazonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
(ruzuku inayojumuisha uhawilishaji pesa, Ujenzi au
ukarabati wa miundombinu na kuimarisha njia za
kujiingizia kipato katika kaya). Msaada wa kiufundi
unatolewa na UNICEF Tanzania na Tume ya Kudhibiti
UKIMWI Tanzania (TACAIDS).